Skip to main content

Utawala Bora

MFUMO WA UTENDAJI WA KAMPUNI

Mfumo wa Utendaji wa Kampuni ya Uwekezaji ya TCCIA inajumuisha fedha zinazopatikana kwa ajili ya kuwekeza kwenye maeneo yaliyoainishwa kwenye Mpango Mkakati wa Kampuni. Kampuni ina matarajio makubwa katika kutimiza malengo yake ya muda mrefu. Kutokana na uimara wa Kampuni, tunaamini kwa siku zijazo inaweza kuwa fursa muhimu katika kuchangia maendeleo na kufanya kazi na wadau wetu kwa kutoa suluhisho la uhakika katika mazingira salama. Maendeleo ya Kampuni ni muhimu sana katika shughuli za biashara, na malengo mapya tuliyojiwekea yatatusaidia kuchukua hatua zaidi. Mafanikio haya yanatokana na uwezo wa Kampuni wa kufanya uwekezaji sahihi na wenye faida. Mfumo wa uendeshaji wa Kampuni yetu unazingatia Kanuni za Utawala Bora.

Kampuni imeendelea kufanya vizuri hata pale thamani ya hisa katika Soko la Hisa inaposhuka thamani kutokana na mpango mkakati na mtaji wake.

 Uongozi Katika Kampuni

Bodi ya Wakurugenzi (Bodi) ni muhimili katika Utawala na inawajibika katika utendaji wa Kampuni. Bodi inaiongoza Kampuni kwa uwazi, uadilifu na kufanya mamuzi ambayo yanasaidia kufikia matarajio ya wanahisa kwa kutimiza majukumu yake vizuri.

Kamati za Bodi

Kwa mfumo wa Bodi wa sasa, kuna Kamati mbili zinazosaidia katika majukumbu mbalimbali.

Wajibu wa Bodi

Bodi inawajibika katika kuiongoza Kampuni, kusimamia biashara, uadilifu na uwajibikaji na kuhakikisha matarajio ya wanahisa yanafikiwa kwa kutimiza majukumu yake vizuri.

Kamati za Bodi

Bodi imekabidhi majukumu kadhaa kwa Kamati. Katiba ya Kampuni imeainisha mambo ambayo yatafanyiwa maamuzi na Bodi na ambayo yatafanyiwa maamuzi na Kamati.  Wajumbe na Wenyeviti wa Kamati kwa kushirikiana na Bodi wamekuwa wakipitia mara kwa mara mwenendo wa Kampuni. Bodi inafahamu kuwa wajumbe wa Kamati kwa pamoja wana sifa za kutosha na uzoefu wa kutimiza majukumu ya Kamati husika. Mwenyekiti anawatathmini wajumbe wa Bodi kupitia taarifa zinazotolewa kila robo mwaka kupitia majadiliano au taarifa zinazowasilishwa kwa maandishi. Wenyeviti wa kamati wanashiriki katika kuandaa Dondoo za Mkutano na kuziidhinisha.

Kamati ya Ukaguzi

Kamati ya Ukaguzi ina Wajumbe watatu ambao sio watendaji wa Kampuni. Afisa Mtendaji Mkuu, Mkuu wa Idara ya Fedha na Mkuu wa Idara ya Utawala wanahudhuria vikao pia.

 

Wajibu wa Bodi kwa Kamati

Ni jukumu la Bodi kusimamia mchakato wa utoaji wa taarifa ya fedha, mfumo wa udhibiti wa ndani, mchakato wa ukaguzi, na kuhakikisha Kampuni inafuata Kanuni na Sheria zilizowekwa.

Majukumu ya Kamati

Jukumu Kuu la Kamati ya Ukaguzi ni;

  • Usimamizi wa Uadilifu katika Utoaji wa Taarifa za Mahesabu.
  • Kupima sifa na utendaji wa Wakaguzi wa nje.
  • Kutoa mwongozo wa Ukaguzi wa ndani wa Kampuni.
  • Kuangalia ufanisi wa Ukaguzi wa Ndani.
  • Kuangalia mfumo mzima wa Utendaji wa ndani wa Kampuni.
  • Kupitia taarifa zinazotolewa na Menejimenti kuhusu mambo yanayoweza kuathiri Kampuni.

Kamati ya Uwekezaji

Kamati ya Uwekezaji inaundwa na wajumbe wawili ambao sio watendaji wa Kampuni. Afisa Mtendaji Mkuu, Mkuu wa Idara ya Fedha na Mkuu wa Idara ya Utawala wanahudhuria vikao pia.

 Wajibu.

Jukumu muhimu la Kamati ya Uwekezaji ni kutoa mwongozo wa mapato na kusimamia Uwekezaji ambao utailetea Kampuni faida kubwa.

Majukumu ya Kamati ya Uwekezaji

  • Kusimamia na kutathmini shughuli za Uwekezaji katika Kampuni kulingana na bajeti.
  • Kuandaa mpango mkakati wa Kampuni wa Uwekezaji na kuishauri Bodi kuiidhinisha.
  • Kuwekeza, Kuandaa mwongozo na viwango vya
  • Kupitia na kukagua matokeo ya uwekezaji katika muktadha wa utendaji kwa kuzingatia kanuni za uwekezaji.
  • Kutoa mwongozo wa uwekezaji kwenye Kampuni ili kupata faida kubwa kulingana na kanuni za Sera ya Uwekezaji kwa kuzingatia muundo, utafiti na athari zinazoweza kujitokeza kulingana na kiwango cha uwekezaji.
  • Kuishauri Bodi kuhusu mapendekezo ya uwekezaji na kusitisha uwekezaji katika biashara na miradi ambayo imeainishwa kulingana na Mpango Mkakati.

Contact info

TCCIA Investment Company Limited [TICL] is a public limited liability company that was established by shareholders to expand financing sources to participate meaningfully in the ownership and control of the Tanzanian economy